SIMBA YA KLABU BINGWA YAMOTO SANA YAMCHAPA MTU SITA

 


Klabu ya Simba imeibuka na ushindi mnono wa goli sita kwa moja dhidi ya Mighty Wonderers ya nchini Malawi, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.

Magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji Clatous Chama 2, Libase Gueye 2, Kaletso Maghlwa 1 na Morice Abraham 1, ikiwa ni mchezo wa marudiano wa ambapo katika mchezo wa kwanza Simba iliibuka na ushindi wa goli moja katika Uwanja wa Bingu, Lilongwe Malawi.

Kwa matokeo haya, Simba inafuzu kwenda katika hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa kwa aggregate ya magoli Saba kwa Moja, ikiisukuma Mighty Wonderers nje ya Mashindano.

No comments