WIZARA YA AFYA YAIMARISHA UWEZO WA WATAALAM KUKABILIANA NA MILIPUKO YA MAGONJWA NA MATUKIO YA DHARURA NCHINI
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa na kuendesha mafunzo kwa Watumishi wa Afya kwa lengo la kuimarisha na kuboresha uchukuaji wa hatua za haraka katika kubaini,kutoa taarifa na kukabiliana na milipuko ya magonjwa na matukio ya dharura yanayoathiri afya nchini.
Akizungumza leo Septemba 28, 2026 jijini Arusha wakati akifungua mafunzo hayo, Dkt.Simon Chacha Mtaalam wa afya ya jamii Wizara ya Afya akimwakilisha Dkt.Erasto Sylvanus Mkurugenzi Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya amesema Wataalam watajengewa uwezo kuhusu mbinu mpya ya kuboresha udhibiti wa utoaji wa huduma za afya ya 7-1-7.
Dkt. Chacha ameeleza kuwa, mbinu hii inatoa lengo la kubaini tukio au ugonjwa kutokea katika kipindi cha siku saba , kutoa taarifa kwa mamlaka ndani ya siku moja kwa ajili ya hatua za udhibiti na namba 7 ya mwisho ni kuchukua hatua za awali za udhibiti ndani ya siku saba.
"Naomba kutoa wito kwa wataalam kutumia vema maarifa mtakayopata katika Mafunzo haya kwenda kuimarisha uchukuaji wa hatua kwa haraka katika kukabiliana na milipuko ya magonjwa pamoja na tishio za mvua za El niño" amesema Dkt.Simon
Vilevile, Dkt.Simon ametoa pongezi kwa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Maambukizi cha Marekani (US CDC) pamoja na Wadau wengine kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Afya katika mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
Ameongeza kuwa,mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili Septemba 28 na 29, 2026 ili kuwajengea uwezo Waratibu wa vituo vya operesheni ya dharura za afya kutoka M
mikoa 26 ya Tanzania Bara, Wataalam kutoka Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.
Akihitimisha Dkt. Chacha amesisitiza kuwa kufanyika kwa mafunzo hayo muhimu ni mwendelezo wa juhudi na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ya Afya katika mapambano dhidi ya milipuko ya magonjwa

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Post a Comment