Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga, amewaomba Vijana kuendelea kulinda amani



Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  Shaibu  Ndemanga, amewaomba Vijana kuendelea kulinda amani ya Taifa kwani kutoka   Uhuru mpaka sasa ni matunda yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Ndemanga ameyasema hayo katika Wiki ya Vijana Kimkoa iliyofanyika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kwenye 

Bonanza  limehusisha shughuli mbalimbali za Kijamii ikiwemo, uchangiaji damu, ufanyaji Usafi, kutoa pole kwa Wagonjwa katika hospital ya Wilaya Bagamoyo na Michezo.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Pwani  Samaha  Said amesema kuwa UVCCM itaendelea kuenzi na kukumbusha vijana umuhimu wa kujitoa na kufanya shughuli zote zinazosisitizwa na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan.


Katika Bonanza la wiki ya vijana kuelekea katika Kilele Cha Mbio za Mwenge 2026, CPA. Subira Mgalu, Mbunge wa Jimbo la   Bagamoyo,   amewakumbusha Vijana Umuhimu wa Amani na  kuchangamkia mkopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali. 


Aidha katika Wiki hiyo ya vijana Mkufunzi na Mratibu wa Makongamano ya vijana Omary Punzi, amefundisha mada ya vijana kujitambua kuishi katika Maadili, Itifaki na Uzalendo.






No comments