TISEZA yataja uwekezaji mpya wa kiuchumi naa ajira Bagamoyo mkoani Pwani
MAMLAKA ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imeeleza kuwa eneo maalum la uwekezaji linaloendelezwa Zinga, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, litafungua fursa kubwa za uwekezaji wa kiuchumi na ajira kwa vijana.
Mradi huo unatekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa hekta 9,800, huku awamu ya kwanza ikilenga kuendeleza maeneo ya kimkakati kwa ajili ya kongani za viwanda na teknolojia.
Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo linaloendelezwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda mbalimbali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema TISEZA inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuweka miundombinu muhimu ili kuwezesha shughuli za uzalishaji.
Nyongo amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Pwani kushirikiana na TISEZA katika kuwaandaa vijana ili waweze kunufaika na fursa zitakazotokana na uwekezaji huo, ikiwemo kuwawezesha kushiriki katika utekelezaji wa asilimia 10 ya fursa zinazotengwa kwa makundi hayo.
Nae Mkurugenzi wa Maeneo Maalum ya Kiuchumi kutoka TISEZA, Anna Lyimo, amesema kati ya viwanda 150 vinavyotarajiwa kuendelezwa katika eneo hilo, ambapo viwanda 25 vimeanza katika hatua mbalimbali za ujenzi, hatua ambayo inatarajiwa kuongeza shughuli za kiuchumi na fursa za ajira katika eneo hilo.






Post a Comment