Mahakama Kuu yapumzika kufanya kazi kuanzia Desemba 15


Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa taarifa kwa Umma na jamii ya wanasheria kwamba kuanzia Desemba 15, 2026 hadi Tarehe 21 Januari, 2027, Mahakama kuu ya Tanzania itakuwa mapumziko. 


Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika kipindi hicho cha mapumziko Mahakama itakaa kwa ajili ya mashauri ya jinai tu na kushughulikia mambo mengine ya dharura.


Pia kwa kipindi hicho, Mahakama za hakimu mkazi na Mahakama za Wilaya, zitasikiliza tu mashauri ya madai yanayowahushisha mawakili na iwapo mashauri hayo ni ya dharura.

No comments