RAIS SAMIA AELEKEA ETHIOPIA,KUZINDUA MPANGO WA AFYA YA MAMA NA MTOTO


Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, anaondoka nchini leo, tarehe 22 Novemba, 2026, kuelekea Addis Ababa, Ethiopia kwa Ziara ya Kikazi ya siku mbili.


Akiwa Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Rais Dkt. Samia, atashiriki Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), na kuzindua Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika, tarehe 23 Novemba,2026.


Mpango huo unalenga kuongoza nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kufikia malengo yajulikanayo kama Sifuri Tatu (Three Zeros), ambayo ni:


1. Kuhakikisha kila mjamzito anajifungulia katika kituo cha kutolea huduma zaafya akisaidiwa na mtaalamu;

2. Kukomesha vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga,vinavyowezakuzuilika;na

3.Kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo.


Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika utatekelezwa kuanzia mwaka 2026 hadi 2030, ukilenga kuongeza uwekezaji wa nchi wanachamana wadau wa maendeleo katika kupanua upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wanawake, watoto na vijana barani Afrika.


No comments