CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM CHATEKELEZA MRADI WA ELIMU YA JUU KWA MAGEUZI YA UCHUMI (HEET) KWA ASILIMIA 80


Chuo kikuu cha Dar es salaam kimeendelea kutekeleza mradi wa elimu ya juu kwa mageuzi ya uchumi (HEET), ambao kwa sasa umefikia asilimia 80 tangu kuanzishwa kwake. mradi huo umelenga kuboresha ubora wa elimu ya juu nchini kwa kujenga mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.

Tayari chuo hicho kimeanza kupata mafanikio mbalimbali ikiwamo ujenzi wa miundombinu ya kisasa, madarasa mapya, na maabara za kisasa zitakazowezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo zaidi.

Ujenzi huo unatarajiwa pia kuambatana na uanzishwaji wa mitaala mipya itakayolingana na mahitaji ya soko la ajira, ili kuongeza ufanisi na ushindani wa wahitimu katika sekta mbalimbali za maendeleo ya taifa.

Umuhimu wa Mradi wa HEET ni mkubwa kwani unalenga kuboresha ubora wa elimu ya juu nchini kwa kujenga miundombinu ya kisasa, kuanzisha mitaala inayolingana na mahitaji ya soko la ajira, na kuongeza ujuzi wa vitendo kwa wanafunzi. Hivyo, mradi huu utachangia kuzalisha wataalamu wabobezi watakaosaidia kuimarisha uchumi wa taifa na kuchochea maendeleo endelevu.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye, alisema mradi huo ni wa kitaifa na umeendelea kuwa chachu ya mageuzi katika elimu ya juu, kwani unalenga kuandaa watalaamu wabobezi watakaosaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.

Aidha, mradi huo umetajwa kuwa na mafanikio makubwa ikiwamo kuimarisha elimu ya juu nchini kwa kiwango cha juu zaidi, kupitia ujenzi wa miundombinu bora, kuongezeka kwa ubora wa ufundishaji na ujifunzaji, pamoja na kuandaa wahitimu wenye ujuzi, ubunifu na uwezo wa kushindana katika soko la ajira la ndani na kimataifa. Mradi huu umekuwa kuwa nguzo muhimu katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi, sambamba na kuinua hadhi ya elimu ya Tanzania.











No comments