JEZI MPYA YA KIMATAIFA YA YANGA HII HAPA


Klabu ya soka ya yanga leo imezindua rasmi jezi mpya kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya CAF.

Awali Meneja wa habari na mawasiliano wa Yanga Ally Kamwe amesema kuelekea katika michezo yao ya makundi ya klabu Bingwa Afrika siku ya alhamisi saa sita watauachia uzi huo na kuwataka mashabiki kujitokeza kununua 

Yanga msimu huu inashiriki ligi ya Mabingwa afrika na imepangwa kundi B ikiwa na timu ya Far Rabat ya Moroco, AL Ahly ya Nchini Misri na JS Kabylie Algeria.

Mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi unatarajiwa kupiigwa siku ya jumamosi visiwani Zanzibar dhidi ya Far Rabat ya Moroco.










 














No comments