UTATA KIFO CHA DADA WA KAZI MAGARI YACHOMWA

Katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, taharuki ilizuka jana Desemba 2025 baada ya magari mawili kuchomwa moto na kuharibiwa na Wananchi waliokuwa wakisindikiza msiba. 


Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Magari hayo yenye namba za usajili T.214 EJU (Mazda CX-5) na T.350 DCH (Toyota Noah), yalikuwa yakisafirisha mwili wa marehemu Mwanahasan Juma Hamis (18), mfanyakazi wa kazi za ndani jijini Dar es Salaam, aliyefariki dunia na kurudishwa nyumbani kwao Turiani kwa ajili ya mazishi.


Taarifa zaidi zimeeleza kuwa tukio hilo lililotokea katika Kitongoji cha Kilinganeni, Kijiji cha Lusanga, Kata ya Diongoya, Tarafa ya Turiani, lilisababishwa na baadhi ya waombolezaji na wakazi wa eneo hilo, ambao walihisi kuwepo kwa mazingira ya kifo kisicho cha kawaida, hali iliyosababisha kuchomwa kwa magari hayo kama njia ya kuonesha hasira.


Aidha, Jeshi la Polisi Mkoani humo limesema linaendelea kushirikiana na Viongozi wa Serikali za Mitaa na Wananchi kwa ujumla ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo, pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria


Taarifa kamili itatolewa mara baada ya uchunguzi kukamilika.

No comments