HUYU HAPA NDIO KOCHA MPYA WA SIMBA?

Tetesi za soka hapa Nchini zinasema kuwa Klabu ya Simba SC hivi karibuni ilikuwa kwenye mazungumzo na kocha Mtunisia Mohamed Sahli, ambaye alikuwa mgombea mkuu wa nafasi ya kocha mkuu, licha ya makocha wengi kuomba kazi Simba Sc ikiwemo aliyekuwa kocha wa watani wao Yanga Sc, Romain Folz.


Tetesi hizo zinakuja kufuatia kufutwa kazi kwa aliyekuwa Meneja Mkuu wa timu hiyo Mbulgaria Dimitar Pantev,  Desemba 2, 2025, na kupelekea timu hiyo kuwa chini ya kocha Msaidizi Selemani Matola, ambapo mchakato wa kutafuta kocha mpya ukiendelea.

Taarifa za hivi karibuni zaidi zinaonyesha kuwa uongozi wa klabu ulikuwa ukiendelea na mchakato wa kumthibitisha kocha mpya na walikuwa wanamjadili sana Mohamed Sahli. 

Tetesi hizo zinakuja siku moja tangu Meneja wa Habari na mawasiliano Klabu ya Simba Ahmed Ally kusema kuwa kabla ya krismasi Klabu hiyo itakuwa imeshapata kocha mpya atakae iongoza timu hiyo.

Mohammed Sahli amezaliwa Aprili 27, 1978 Nchini Tunisia akiwa na uraia wa Austria na ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka akipita vilabu kadhaa vya Ujerumani (Bundesliga) ikiwemo Wolfberg na Us Monastir ya Algeria.


No comments