JENISTA AWAKUTANISHA KIKWETE MPANGO NA MAJALIWA.

Baadhi ya viongozi wakuu wastaafu wa Tanzania, akiwemo Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete; Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango; pamoja na Mawaziri Wakuu wastaafu, Kassim Majaliwa na Mizengo Pinda, wameshiriki misa katika Kanisa Katoliki, Kiwanja cha Ndege, jijini Dodoma, ikiwa ni misa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama.


Jenista alifariki dunia Desemba 11, 2025, jijini Dodoma. Baada ya kuagwa leo, mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijiji cha Ruanda, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Desemba 16, 2025.

No comments