KOCHA MPYA SIMBA KUPATIKANA KABLA YA KRISMASI
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ametoa wito kwa wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kumlinda kocha wa muda wa sasa wa klabu hiyo Selemani Matola kwa sababu ni hazina kubwa na amekuwa klabuni hapo kwa muda mrefu sasa.
"Matola amefanya kazi yake ipasavyo, anakwenda vizuri na ni mhimili muhimu kwenye Simba. Tunaweza kumchukulia kwa wepesi Matola kwa sababu tumemzoea, amekaa muda mrefu hapa ni mswahili mwenzetu,"
"Selamani Matola ni moja kati ya hazina kubwa kwenye Simba yetu hii. Mimi niwaambie wanasimba kama kuna vitu tunatakiwa kuvilinda ni pamoja na Selemani Matola".
Ahmed Ally amesema hayo leo Desemba 13, 2025 katika Kipindi cha Jambo Wikendi cha TBC1.

Post a Comment