MRADI WA OPEC WAACHA TABASAMU KIJIJI CHA NGABOBO MKOANI ARUSHA



Zaidi ya wananchi elfu 4 wa kijiji cha Ngabobo katika halmashauri ya Meru Mkoani Arusha wamenufaika na mradi wa mfereji wa umwagiliaji Maji katika kijiji hicho.

Hayo yamebainishwa na Afisa Kilimo wa Kata ya Ngabobo  Godvoice Mbokoi, halmashauri ya Meru Mkoani Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari kijijini hapo.

Mbokoi amesema kuwa kupitia mradi huo wa Mfereji wa umwagiliaji umesaidia kuongeza kipato kwa wakulima katika kijiji hicho kwani wakulima waliokuwa wakilima heka moja awali sasa wanaweza kulima hadi heka tatu mpaka nne na kujiongezea kipato.

Ameongeza kuwa mradi huo wa umwagiliaji umeondoa migogoro miongoni mwa wakulima wa kijiji hicho .

Amesema awali ilikuwa kuna malalamiko kwa baadhi wa Wakulima kutopata maji ila baada ya mradi huo wakulima wote wamekuwa wakipata maji na kumwagilia mazao yao.

Mradi huo wa Mfereji wa Umwagiliaji unatekelezwa  kupitia mradi wa Opec kupitia Mfuko wa Maendeleo ya jamii nchini Tasaf.

Mradi wa Opec umefikia ukingoni Desemba 31 mwaka 2025



No comments