RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN ATUMA SALAMU KIFO CHA ALIYEKUWA GAVANA BOT

 


Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mzee Edwin Mtei, Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mzee Mtei atakumbukwa kwa mchango wake muhimu katika ujenzi wa Taifa letu, hususan katika kuimarisha misingi ya mipango, uchumi, fedha na demokrasia.



Ninatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. 




No comments