MUHIMBILI YAWEKA KAMBI YA MATIBABU YA MACHO KWA WATUMISHI WA TANZANIA EAST AFRICA GATEWAY TERMINAL LIMITED
Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga&Mloganzila) imeendelea na juhudi za kuunga mkono Serikali kwa kusogeza karibu huduma za ubingwa na ubobezi kwa jamii kwa kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya macho kwa watumishi wa Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL) .
Kampuni hiyo inasimamia na kuendeshea kituo cha kontena namba 2 (CT2) , kinachojumuisha Gati namba 8 hadi 11 katika Bandari ya Dar es Salaam,hatua inayolenga kuboresha afya za wafanyakazi bila kuathiri majukumu yao ya kazi.
Daktari Bingwa wa Macho kutoka MNH,Dkt. Johaness Mafwiri amesema huduma zinazotolewa ni uchunguzi wa awali, matibabu pamoja na ushauri wa kitaalamu kuhusu namna ya kulinda afya ya macho ambapo watumishi watakaobainika kuwa na changamoto zinazohitaji ufuatiliaji zaidi watapew rufaa ya kwenda Muhimbili kwa uchunguzi wa kina na matibabu ya ubingwa.
Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Muhimbili wa kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi, hususani wafanyakazi walioko katika taasisi mbalimbali za Umma na binafsi ili kuwawezesha kupata huduma kwa urahisi na kwa wakati muafaka.
Kupitia mpango huo, wataalamu wa Muhimbili wamekuwa wakitembelea kampuni, taasisi binafsi na mashirika ya serikali kutoa huduma za uchunguzi, matibabu na elimu ya afya. Hatua hii imeongeza uelewa kwa wafanyakazi kuhusu umuhimu wa uchunguzi wa mara kwa mara na kuchukua hatua mapema dhidi ya magonjwa mbalimbali ya macho.
Huduma hizi zinaendelea kuimarisha dhamira ya Muhimbili ya kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia wananchi popote walipo, huku zikichangia kuboresha afya na ustawi wa watumishi pamoja na kuongeza tija katika maeneo yao ya kazi.

Post a Comment