SIMBA SC, KMC FC KUANZA SAFARI YA KUTAFUTA NAFASI YA KIMATAIFA KUPITIA MICHUANO YA FA LEO.



Kikosi cha Simba leo kinatarajia kutupa karata yake ya kwanza katika mchezo wa kombe la shirikisho la Tanzania  CRDB FA CUP dhidi ya Greenland Fc ya mkoani Kagera.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa moja usiku katika uwanja wa meja issamuyoh mbweni Jijini Dar es salaam

Simba unakuwa mchezo wake wa kwanza baada ya kuondoshwa katika michuano ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi wakiwa wamekusanya alama tano pekee msimu huo ambazo zimeshindwa kuwafikisha katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Simba itaendelea kukosa huduma ya wachezaji wake Abdulazaq Hamza ambae anamajeraha ya muda mrefu na anatarajiw akuakaa nje kwa msimu mzima wa 2025/2026. wengine ni watakaokosekana ni pamoja na wilson Nangu majeraha na Shomari Kapombe, Jonathan Sowah, Allasane Kante kwa sababu mbalimbali

Mchezo wa mapema utapigwa saa kumi jioni katika dimba la Kmc ni kati ya Kmc VS Bandari Tanzania.

No comments