JAMII YAKUMBUSHWA KUWAHESHIMU NA KUWAJUMISHA WATU WENYE DOWN SYNDROME KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Down Syndrome,yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuikumbusha jamii kuhusu wajibu wa kuhakikisha usawa, heshima na ujumuishwaji wa kundi hilo katika nyanja zote za maisha.
Machi 21 kila mwaka,dunia huungana kutafakari mchango wa watu wenye hali hiyo, huku Tanzania nayo ikiungana na mataifa mengine kuadhimisha siku hiyo kwa lengo la kuongeza uelewa na kuondoa changamoto wanazokutana nazo.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hay oleo Jijini Dodoma,Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Watu Wenye Ulemavu Kizito Wambura amesema kwa mwaka huu maadhimisho hayo hapa nchini yanafanyika katika ngazi ya halmashauri.
Amebainisha hatua mbalimbali ambazo serikali imeendelea kuzichukua katika kuhakikisha watu wenye uleamvu wanapata haki na fursa sawa, ikiwemo kuwepo kwa Sheria ya Watu Wenye Ulemavu, pamoja na sera mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha yao ikiwemo sera ya elimu na mafunzo yam waka 2014 inayosisitiza elimu jumuishi.
Hata hivyo, amesema pamoja na jitihada hizo, bado jamii ina wajibu mkubwa wa kuwatambua, kuwaheshimu na kuwajumuisha watu wenye Down Syndrome katika shughuli zote za maendeleo,huku akitoa wito kwa wadau wote kushirikiana kujenga jamii yenye usawa, haki na mshikamano bila ubaguzi.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Tuwe Pamoja Dhidi ya Upweke” ikilenga kuhimiza jamii kushirikiana katika kuwajumuisha watu wenye Down Syndrome na kuwaondolea ubaguzi.
Post a Comment