TRA KUENDELEA KURAHISISHA UINGIZAJI WA MAFUTA YA VYOMBO VYA MOTO SOKONI
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema Mamlaka hiyo itaendelea kuwezesha utolewaji wa haraka wa mafuta ya Petroli na Dizeli kwenye vituo vya kuhifadhia bidhaa hizo kwenda sokoni.
Akizungumza katika kikao baina yake na Viongozi wa Umoja wa Wamiliki wa Vituo vya Mafuta ya Petroli na Dizeli nchini (TAPSOA) kilichofanyika Machi 24, 2026 kwenye ofisi za TRA jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuendelea kuwezesha biashara hiyo, Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA haipo tayari kuona ucheleweshaji wa bidhaa hiyo kuingia sokoni ukifanyika.
Aidha amesema TRA itaendelea kuleta usawa katika biashara ya mafuta hayo nchini ili kweka ushindani ulio sawa sokoni kwa kudhibiti uchepushaji wa shehena za mafuta unaofanywa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA itaendelea kuwezesha biashara ya mafuta nchini ili iendelee kufanyika kwa ufanisi na kusikiliza changamoto zinazowakabili wamiliki wa Vituo vya mafuta na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.
Akizungumza katika kikao hicho Katibu wa TAPSOA Bw. Tino Mmasi amemshukuru Kamishna Mkuu wa TRA kwa kuendelea kuwasikiliza na kutatua changamoto zao huku akiahidi kuwa Wamiliki wa Vituo vya mafuta nchini wataendelea kulipa kodi kwa hiari na kushirikiana na TRA kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi.
Post a Comment