OPEC+ YAONGEZA UZALISHAJI KUFUATIA MVUTANO MPYA NA IRAN


 

Wanachama muhimu wa shirika la wazalishaji wakubwa wa mafuta ulimwenguni, OPEC+, wametangaza ongezeko kubwa kuliko ilivyotarajiwa la uzalishaji wa mafuta.

Hatua hii ni kufuatia mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran na hatua za kulipiza kisasi za Iran Mashariki ya Kati.

Kundi la mataifa Nane ndani ya muungano huo, ikiwemo Saudi Arabia, Urusi na mataifa kadhaa ya Ghuba yaliyolengwa na makombora ya Iran, limesema limekubaliana kuongeza uzalishaji kufikia mapipa laki mbili na elfu sita kwa siku kuanzia ,mwezi ujao.

Hata hivyo, wachambuzi wanaonya kuwa ongezeko hilo halitoshi kuzuia kupanda kwa bei, hasa ikiwa Iran itafunga mlango-Bahari wa Hormuz, njia inayopitisha karibu robo ya mafuta ya dunia.

Kufungwa kwa Hormuz hata kwa siku chache kunaweza kupandisha bei hadi kati ya dola 120 na 150 kwa Pipa. 

Wataalamu wanasema Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu wana njia mbadala za mabomba, lakini bado kutabaki na upungufu mkubwa sokoni.

No comments