SERIKALI YAPENDEKEZA KUKUSANYA NA KUTUMIA SH. TRILIONI 62.334 KWA MWAKA WA FEDHA 2026/27

 


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27, ambapo katika kipindi hicho, inatarajia kukusanya nakutumia shilingi trilioni 62.334 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, maendeleo na kulipia deni la Taifa.


Mhe. Balozi Omar amesema hayo wakati akiwasilisha Mpango huo ambapo amesema kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 10.3 ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2025/26.


Tukio hilo limeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa pia na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu, na viongozi waandamizi wa Serikali.





No comments