TPDC YAONGEZA UPATIKANAJI WA GESI ASILIA NA KUPANUA WIGO WA USAMBAJI MAFUTA
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC),katika Mwaka wa fedha wa 2025/2026,inaendelea kutekeleza miradi nane inayolenga kuongeza upatikanaji wa gesi asilia,kupanua wigo wa usambazaji wa mafuta na gesi asilia wakati ikizingatia utekelezaji wa miradi ya CSR na ushirikishwaji wa wazawa katika mnyororo wa thamani wa sekta ya mafuta na gesi.
Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP),ambao umefikia asilimia 81 ya utekelezaji na ujenzi wake unatarajiwa unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2026.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC,Mussa Mohammed Makame,amesema hayo Machi 11,2026,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya shirika hilo pamoja na fursa zinazotolewa kwa vijana katika mwaka wa fedha wa 2025/2026.
Amesema miradi hii yote si tu kwamba inachochea ukuaji wa uchumi wa Taifa, bali pia inafungua milango ya ajira, ujuzi na ushiriki wa vijana katika sekta ya nishati.
“Ni muhimu kufahamu kuwa takribani asilimia 79 ya nguvu kazi ya TPDC ni vijana ambao kwa vipindi tofauti wamekuwa wakijengewa ujuzi wa masuala mbalimbali ya kuendesha sekta ya nishati,hiyo inaonesha dhamira ya Serikali katika kuwakuza, kuwaamini na kuwapa nafasi vijana wa Kitanzania kuongoza sekta hii ya kimkakati,”amesema.
Ametaja mradi mwingine kuwa ni wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia kuwa kimiminika (LNG), unaotarajiwa kugharimu takribani Dola za Marekani bilioni 42,ambapo serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha mazungumzo ya utekelezaji wake.
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment