WABUNIFU MAJENGO WAANDAA SEMINA YA MAENDELEO YA MIJI
Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania kimetangaza kuandaa semina itakayojadili maendelezo ya miji yaliyopangwa kwa kuzingatia mipango miji katika miji mbalimbali nchini.
Semina hiyo itafanyika Aprili 9 hadi 10 mwaka huu mkoani Morogoro na inatarajiwa kuwakutanisha wataalamu mbalimbali wa sekta ya ujenzi wakiwemo wahandisi, wabunifu majengo, wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na wadau wengine wa maendeleo ya miji.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya semina hiyo, Rais wa Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania, Mecky Chawi amesema lengo la mkutano huo ni kujadili namna bora ya kupanga na kuendeleza miji ili iendane na kasi ya ukuaji wa miji nchini.
Amesema semina hiyo itatoa fursa kwa wataalamu kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto za upangaji wa miji na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha maendeleo ya miji nchini.
Aidha amesema kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 600 kutoka maeneo mbalimbali nchini watakaoshiriki katika mijadala na mada mbalimbali zitakazowasilishwa wakati wa semina hiy
Post a Comment