SERENGETI BOYS YAONDOKA KWENDA MISRI KUJIANDAA NA AFCON U17 2026
Timu ya Taifa ya wavulana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, imeondoka nchini kuelekea Misri kwa ajili ya kuweka kambi maalum ya maandalizi kuelekea mashindano ya TotalEnergies U-17 Africa Cup of Nations 2026.
Mashindano hayo makubwa ya vijana barani Afrika yanatarajiwa kufanyika nchini Morocco, ambapo Serengeti Boys inatarajia kutumia kambi hiyo kuimarisha maandalizi kuelekea mashindano hayo.
Kambi hiyo ya maandalizi nchini Misri inalenga kuwapa wachezaji uzoefu zaidi wa kimataifa, kuimarisha mbinu za kiufundi na kuongeza uimara wa kikosi kabla ya kuingia kwenye mashindano hayo muhimu ya vijana barani Afrika.
Mashindano ya AFCON U17 pia hutumika kama jukwaa la kutambua vipaji chipukizi vinavyoweza kuja kuwa nyota wa baadaye wa soka la Afrika na dunia.
Post a Comment