WANANCHI WANAYO MATUMAINI MAKUBWA NA REA
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi, Hassan Saidy, amesema wananchi hususan wanaoishi vijijini wana matumaini na Serikali kupitia REA katika kuwaboreshea hali ya maisha na amewataka Watumishi wa Wakala kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii, uadilifu na maarifa ili kutimiza malengo ya Serikali kuhudumia wananchi wake.
Ametoa rai hiyo mjini Morogoro wakati wa kufungua Kikao cha Tatu cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa REA lenye ajenda kuu ya Kupitia na Kujadili Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2026/2027.
Amesema makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti kwa Mwaka 2026/2027 yanayojadiliwa katika Baraza hilo yamelenga kuboresha mazingira ya kazi na uwezo wa Taasisi katika kutekeleza majukumu yake sambamba na maslahi ya Watumishi.
Akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa ndani ya kipindi cha miezi 12 (kutoka kikao cha Baraza kilichopita cha Mwezi Machi, 2025 hadi kikao cha sasa Machi, 2026), Saidy amesema REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye vitongoji 3,532 ambayo ni sawa na wastani wa vitongoji 10 kwa siku.
Katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), Hery Mkunda ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uzalendo.
Post a Comment