WASHIRIKA WA MAREKANI KATIKA ENEO LA GHUBA WANAHUSIKA NA MASHAMBULIZI YA IRAN

 


Wizara ya ulinzi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imesema hadi sasa "imeshughulikia" makombora 165 ya balestiki, makombora mawili ya baharini na ndege zisizo na rubani 541 za Iran.

 

Huko Bahrain, Jumapili asubuhi uwanja wa ndege umeshambuliwa.

 

Haya si matukio ya kawaida katika eneo hili, lakini tangu mzozo huu uanze Jumamosi asubuhi, Iran inaonekana kupanua lengo lake kutoka kwa shabaha za kijeshi, kama vile makao makuu ya Jeshi la Wanamaji la Marekani nchini Bahrain, hadi viwanja vya ndege na maeneo mengine ya kiraia.

 

Sasa hoteli za kifahari na maduka makubwa, majengo ya ghorofa ya juu, vituo vya juu vya ndege vinaathirika mara kwa mara huku mapengo yakionekana katika ulinzi wa anga wa mataifa ya Kiarabu katika Ghuba.

 

Maeneo haya hayakuwahi kujengwa kwa matarajio akilini kwamba siku moja yatashambuliwa na ndege zisizo na rubani na makombora ya balestiki.

No comments