MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA DOWEICARE, WAGAWA TAULO ZA KIKE 6,000
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Mwang’onda, ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha Doweicare Technology Limited kilichopo Misugusugu, Kibaha mkoani Pwani, huku akipongeza serikali kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, hali inayochochea ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.
Kiwanda hicho kinazalisha bidhaa za usafi zikiwemo nepi za watoto na taulo za kike, kikiwa kimewekeza takribani shilingi bilioni 40.
Katika hatua nyingine, Mwang’onda amegawa taulo za kike elfu sita kwa wanafunzi elfu moja, zitakazowasaidia kwa kipindi cha miezi sita.
Aidha, Mwang'onda ameipongeza Manispaa ya Kibaha kwa ushirikiano wake na serikali katika kuimarisha uwekezaji na maendeleo ya viwanda.
Awali, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa, amesema jumla ya miradi nane yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 41 imezinduliwa, kukaguliwa na kuwekwa mawe ya msingi.
Miradi hiyo ni pamoja na barabara ya Kongowe hadi Forest, vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Picha ya Ndege, huduma za afya katika Zahanati ya Kilimahewa, pamoja na mradi ya maji .
Mwenge wa Uhuru uko katika siku ya nne tangu kuwasili mkoani Pwani na unatarajiwa kuendelea na mbio zake wilayani Mafia Aprili 22, 2026.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


Post a Comment