KATIBU MKUU CCM, UJUMBE MTANDAO WA VIONGOZI WANAWAKE AFRIKA WAFANYA MAZUNGUMZO


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Asha-Rose Migiro, leo tarehe 21 Aprili 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Mtandao wa Viongozi Wanawake wa Afrika (African Women Leaders Network - AWLN), ulioongozwa na Marais wastaafu wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, na Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Sahle-Work Zewde, jijini Dar es Salaam.


Mazungumzo hayo yalijikita katika hali ya kisiasa nchini pamoja na matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, yakihusisha pia umuhimu wa kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa.


Ujumbe huo upo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kufanya mashauriano na viongozi mbalimbali wa kitaifa kuhusu maendeleo ya kisiasa na juhudi zinazoendelea za kuimarisha demokrasia na utawala bora, ikiwa ni sehemu ya mchango wa wanawake viongozi wa Afrika katika kulinda amani na utulivu barani.





No comments