KIHONGOSI AWASILI MARA, ASISITIZA AMANI
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi, Kenani Kihongosi, amewasili Musoma Mkoani Mara kwa ziara ya siku tatu mkoani humo.
Kihongosi, amepokelewa katika eneo la Nyabange na kisha kuelekea Ofisi ya CCM mkoa wa Mara na baadaye kutembelea Shina namba tano, mtaa wa Veta Kata ya Mwisenge, Mjini Musoma.
Kihongosi, amesisitiza kuendelea kuilinda amani nchini kwani itakapotoweka hakuna chochote kinachoweza kufanyika.
Awali, mmoja ya wazee wa Kata ya Mwisenge, amemuomba Mwenezi kuiangalia barabara inayoelekea Shule ya Msingi Mwisenge ambayo alisoma baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ili ifanyiwe ukarabati.
Akijibu ombi hilo, Kihongosi, ameahidi kulishughulikia suala hilo kwa kuwasiliana na Serikali ili jambo hilo lipatiwe ufumbuzi.
Anaendelea na ziara Mjini Musoma ambapo anakagua miradi mbalibali inayotekelezwa ikiwemo Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere.




Post a Comment