ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU YATAJWA MUHIMU KULINDA MASLAHI YA WAVUVI MAFIA



Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeendesha mafunzo ya uzingatiaji wa haki za binadamu katika ufikiaji, upatikanaji na usimamizi wa rasilimali za bahari kwa wavuvi wadogo, vikundi vya kina mama wachakataji wa samaki, Chama cha Wanawake Wavuvi Tanzania (TAWFA) pamoja na Kamati za Usimamizi wa Fukwe (BMU) wilayani Mafia.


Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ofisi za Uvuvi eneo la Bondeni Pwani, kijiji cha Kilindoni, yamelenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika matumizi na usimamizi wa rasilimali za bahari.


Ofisa Uchunguzi Mkuu kutoka Tume hiyo, Jovina Mchunguzi ameeleza, elimu ya haki za binadamu ni jukumu la wadau wote na si Tume pekee, hivyo amewahimiza wadau kushirikiana katika kufikisha elimu hiyo kwa wananchi.


Ofisa Uvuvi wa Kilindoni, Jedia Joseph, ameeleza mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza uelewa wa wananchi katika kutambua haki zao na kuleta mabadiliko chanya katika shughuli zao za kila siku.


Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Silima Juma, Katibu wa Kamati Ndogo ya Hifadhi kutoka kijiji cha Kiegeani, amefafanua mafunzo hayo yamewapa mwamko mpya wa kutambua na kutetea haki zao.








No comments