WAZIRI NDEJEMBI AZINDUA KITUO CHA KUCHAJIA VYOMBO VYA USAFIRI VYA UMEME – DODOMA
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua Kituo cha Kuchajia Vyombo vya Usafiri Vinavyotumia Umeme katika Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) jijini Dodoma.
Uzinduzi huo umefanyika Juni 11,2026,ukiambatana na utiaji saini na uzinduzi wa miradi ya nishati safi, ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Vituo vya Kuchajia Vyombo vya Usafiri Vinavyotumia Umeme (EV Charging Stations) pamoja na Mpango wa Ukopeshaji wa Majiko ya Umeme kwa Wateja wa TANESCO (On-Bill Financing – OBF), uliofanyika katika Viwanja vya Mashujaa, Jamatini jijini Dodoma.
Mradi huo unalenga kuboresha maisha ya wananchi na wateja wa TANESCO kupitia upatikanaji wa nishati safi ya umeme, nafuu na yenye ufanisi katika sekta za usafirishaji na matumizi ya kupikia.







Post a Comment