DKT. ABBAS ATEMBELEA BANDA LA MALIASILI MAONESHO YA 50 YA SABASABA 2026
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas ametembelea na kukagua mabanda ya Idara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Katika ukaguzi huo Dkt. Abbas ameongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Maonesho hayo kwa upande wa Wizara, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ernest Mwamwaja, maofisa kutoka wizarani na taasisi zilizo chini ya Wizara.
Katibu Mkuu huyo ametembelea zaidi ya madawati 30 yanayotoa taarifa mbalimbali za Wizara, zikiwemo taarifa za vivutio mbalimbali vya utalii, na uhifadhi hususani katika Maonesho hayo yanayofanyika katika kipindi cha kuelekea Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ( AFCON 2027) ambapo Tanzania inatazamiwa kupokea ugeni mkubwa kupitia tukio hilo la kihistoria.
Pamoja na Tanzania, mataifa mengine wenyeji wa Michuano hiyo ya AFCON ni Uganda na Kenya.
Maonesho ya Sabasaba yalianza rasmi Juni 28, 2026 na yanatarajia kumalizika Julai 13,2926, huku viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa wakitazamiwa kutembelea Maonesho hayo hususani Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.

Post a Comment