HAKI YA MLIPAKODI NI KIPAUMBELE CHETU - MKURUGENZI WA SHERIA TRA
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Elisha Shigella amesema TRA kupitia Idara hiyo imelipa kipaumbele suala la haki kwa walipakodi kwa kuhakikisha kuwa kodi inakusanywa kwa haki na kwa kufuata misingi ya sheria ili mlipakodi alipe kodi stahiki na serikali ipate mapato stahiki kwa maendeleo ya Taifa.
Ameyasema hayo leo Julai 22, 2026 jijini Dodoma alipokutana na watumishi wa Idara ya huduma za kisheria wa TRA nchi nzima.
“Haki ya mlipakodi ni kipaumbele chetu kwa kuhakikisha kodi inakusanywa kwa haki na kwa kufuata misingi ya Sheria” amesema Bw. Shigella
Bw.Shigella amesema Idara ya huduma za Kisheria ndani ya TRA ina jukumu la kuhakikisha misingi ya sheria inafuatwa katika nyanja zote za ukusanyaji mapato ya serikali, pia Idara hiyo inashughulikia mashauri yote ya kikodi ili kuhakikisha kuwa mlipakodi analipa kodi stahiki na serikali inapata kodi stahiki kwa maendeleo ya taifa.
Aidha Bw. Shigella amewataka wanasheria wa Idara hiyo kuhakikisha wanawasaidia walipakodi kisheria pale wanapopata mkanganyiko au kutaka ufafanuzi wa kisheria juu ya mambo mbalimbali ya kikodi ili kuchochea ulipajikodi wa hiari kwa maendeleo ya Taifa.













Post a Comment