𝗠𝗞𝗘𝗡𝗗𝗔 𝗔𝗦𝗛𝗜𝗥𝗜𝗞𝗜 𝗠𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗢 𝗪𝗔 𝗚𝗣𝗘 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗖𝗛𝗔𝗡𝗚𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗥𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗠𝗔𝗟𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗝𝗜𝗟𝗜 𝗬𝗔 𝗘𝗟𝗜𝗠𝗨
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.
Adolf Mkenda, ameshiriki mkutano wa GPE Multiplier Possibility wenye lengo la
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuimarisha elimu duniani, uliofanyika katika
ECOSOC Chamber, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), New York, Marekani.
Mkutano huo umeongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Global
Partnership for Education (GPE), Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkutano huo umejikita katika juhudi za kutafuta na
kuhamasisha rasilimali kutoka kwa wadau wa elimu duniani kupitia mfuko wa GPE,
kwa lengo la kusaidia nchi wanachama kuimarisha na kufadhili miradi mbalimbali
ya elimu.
Kupitia mpango huo, wadau wa elimu duniani
wanahamasishwa kutoa michango itakayowezesha kuongeza uwekezaji katika sekta ya
elimu, hususan katika maeneo yanayohitaji rasilimali zaidi kwa ajili ya
kuboresha upatikanaji na ubora wa elimu.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazowanufaika na
ufadhili wa Global Partnership for Education (GPE), unaolenga kusaidia nchi
katika kuimarisha mifumo ya elimu na kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo
ya elimu.

.webp)
.webp)
Post a Comment