BoT YATOA ELIMU YA UCHUMI NA FEDHA KATIKA TAMASHA LA FAHARI YA ZANZIBAR
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inashiriki katika Tamasha la Tatu la Fahari ya Zanzibar, linalofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, kuanzia tarehe 04 hadi 14 Septemba 2026.
Tamasha hilo lilifunguliwa rasmi tarehe 5 Septemba 2026 na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, ambaye pia alipata fursa ya kutembelea banda la Benki Kuu.
Ushiriki wa Benki Kuu katika tamasha hilo unalenga kutoa elimu na uelewa kwa wananchi kuhusu majukumu ya Benki Kuu, hususan katika kusimamia na kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi, pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya fedha.
%20inashiriki%20katika%20Tamasha%20la%20Tatu%20la%20Fahari%20ya%20Zanzibar,%20linalofanyi.jpg)
%20inashiriki%20katika%20Tamasha%20la%20Tatu%20la%20Fahari%20ya%20Zanzibar,%20linalofanyi%20(2).jpg)
%20inashiriki%20katika%20Tamasha%20la%20Tatu%20la%20Fahari%20ya%20Zanzibar,%20linalofanyi%20(1).jpg)
Post a Comment