WIZARA YA AFYA NA WHO KUWAJENGEA UWEZO KWA VITENDO TIMU YA KITAIFA HUDUMA YA DHARURA



Wizara ya Afya, kupitia kitengo cha Dharura kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), inaendelea kuwajengea uwezo kwa vitendo Timu ya Kitaifa itakayotoa huduma kipindi cha dharula na majanga (EMT) kuhusu afua mbalimbali za kujikinga na kukabiliana na maambukizi ikiwemo utumiaji sahihi ya Vifaa kinga (PPE), usafi wa mazingira na usibuaji pamoja na umuhimu wa upatikanaji wa maji safi na salama katika vituo vya afya na wakati wa utoaji huduma katika dharura na majanga.


Mafunzo hayo yamefanyika leo Septemba 8, 2026 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo yanayofanyika jijini Mwanza yanayolenga kuimarisha usalama watumishi hao na kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya.


Aidha, wawezeshaji wa mafunzo hayo wamewasisitiza wataalamu kuzingatia miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya na kuwa makini wakati wote wa kutekeleza majukumu yao ili kuepuka hatari ya maambukizi kwao wenyewe na kwa wataalamu wenzao katika maeneo ya kazi na wakati wa kutoa huduma za dharura.


Katika mafunzo hayo, wataalamu pia wamepewa ujuzi wa kukokotoa kiasi cha maji na salama kinachohitajika kwa kuzingatia idadi ya watumishi pamoja na idadi ya wagonjwa katika kituo cha afya au wakati wa kutoa matibabu ya  dharura na majanga.


 Pia Wataalmu hao wa Afya wamejengewa uelewa kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira katika kupunguza hatari ya maambukizi kusambaa katika mazingira yanayozunguka vituo vya afya.






















No comments