DKT. ABBASI AKUTANA NA IDARA YA WANYAMAPORI, ASISITIZA UWAJIBIKAJI NA MAADILI KAZINI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Septemba 3, 2026 amekutana na watendaji wa Idara ya Wanyamapori katika mwendelezo wa utaratibu wake wa kawaida wa kukutana na kila Idara na vitengo vya Wizara.
Kikao hicho kimekuwa fursa ya kujadili mipango na vipaumbele vya Idara, kubaini changamoto zinazokabili utekelezaji wa majukumu pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji na ufanisi wa kazi.
Katika kikao hicho, Dkt. Abbasi amesisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili, uwajibikaji na kuzingatia utu katika utendaji wa kazi, akiwataka watendaji kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutimiza kwa wakati yale yaliyoahidiwa, akieleza kuwa utekelezaji wa ahadi na majukumu kwa wakati ni sehemu muhimu ya kujenga taasisi yenye ufanisi na kuleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi.
Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Ndug. Nkoba Mabula.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment