SERIKALI YAANDAA UTEKELEZAJI WA ELIMU YA LAZIMA YA MIAKA 10.
SERIKALI imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha sekta ya elimu kwa kuongeza miaka ya elimu ya lazima, kupanua fursa za elimu ya sekondari na kuimarisha mafunzo ya ufundi, ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika soko la ajira.
Akizungumza Septemba 2, 2026 jijini Dodoma na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema maandalizi ya utekelezaji wa elimu ya lazima ya miaka 10 kuanzia mwaka 2028 yanaendelea.
Amesema utekelezaji wa mpango huo utahitaji uwepo wa miundombinu, walimu na nafasi za kutosha katika shule za sekondari, kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi watakaoingia katika elimu hiyo.
Prof. Mkenda amesema Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili wanapata nafasi ya kuendelea na masomo, wakati huo huo ikiendelea kuimarisha mfumo wa elimu wenye mikondo ya elimu ya jumla na elimu ya amali.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema Serikali inatazama uwezekano wa kuboresha vivutio vya kisera vitakavyoongeza uwekezaji wa sekta binafsi katika sekta ya elimu.
Naye Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Marianne Young, amepongeza juhudi zinazofanywa na Tanzania katika kuimarisha elimu na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika elimu na mafunzo ya ufundi.
.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)

Post a Comment