KADOGOSA 'AULA' ATEULIWA WAZIRI WA UJENZI
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kungu Kadogosa, ambaye kwasasa ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini mkoani Simiyu, kupitia chama cha Chama cha Mapinduzi (CCM) ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Ujenzi, akichukua nafasi ya Abdallah Hamis Ulega, ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Uteuzi huo umetangazwa Jumapili, Septemba 27, 2026, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.
Kadogosa anaingia katika nafasi hiyo akiwa na uzoefu wa muda mrefu katika sekta ya miundombinu, hususan kwenye masuala ya reli na usafiri. Kabla ya kuingia katika siasa, aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika sekta ya fedha na reli.
Akiwa Waziri wa Ujenzi, Kadogosa atakuwa na jukumu la kusimamia sekta inayohusisha ujenzi na maendeleo ya barabara, madaraja pamoja na miradi mbalimbali mikubwa ya miundombinu nchini.
Uteuzi wake unakuja wakati ambapo miradi ya miundombinu ikiendelea kuwa sehemu muhimu ya ajenda ya maendeleo ya Tanzania, hivyo utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo utakuwa miongoni mwa maeneo yatakayokuwa chini ya wizara hiyo.



Post a Comment