YANGA YASIKITIKA KUMPOTEZA MZEE MPILI
Uongozi wa Klabu ya Yanga (Young Africans Sports Club), unasikitika kutangaza kifo cha mwanachama wake, Haji Ramadhani Mpili, maarufu Mzee Mpili, kilichotokea usiku wa Tarehe 27, Septemba 2026 katika Kituo cha Afya Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani alipokuwa akipatiwa Matibabu.
Kupitia ukurasa wao wa Instagram @yangasc wamesema mazishi yanatarajia kufanyika saa kumi jioni katika Makaburi ya Msikiti Mkubwa, Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.
Uongozi wa Yanga, unatoa pole Kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa Mpira na kuwaomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina


Post a Comment