WANANCHI ZANZIBAR KUUNGANISHWA NA INTANETI NDANI YA MIAKA MITATU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inalenga kuunganisha kaya 100,000 na huduma za intaneti kupitia mfumo wa Fibre-to-the-Home ndani ya miaka mitatu, huku ikiandaa Mfumo Mkakati wa Akili Unde (AI Strategy Framework) utakaoongoza matumizi salama na yenye uwajibikaji ya teknolojia hiyo.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 29 Septemba 2026, wakati akifungua Maonesho ya Teknolojia na Akili Unde (Tech and AI Expo Zanzibar 2026) katika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar, sambamba na uzinduzi wa Sera ya Kidijitali ya Zanzibar 2026.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejizatiti kuendeleza mageuzi ya kidijitali kwa kuimarisha miundombinu, kuongeza matumizi ya teknolojia katika huduma za umma na uchumi, pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana, wabunifu na wawekezaji.
Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kimkakati (MoU) baina ya Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar na Huawei Technologies Tanzania Limited.

Post a Comment