MADEREVA WA MABASI WAGOMA DODOMA



Madereva wa mabasi yanayofanya safari kutoka Mkoani Dodoma kwenda mikoa mbalimbali nchini wamesitisha huduma ya usafirishaji wa abiria, wakitaka serikali kushughulikia changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.


Miongoni mwa mambo wanayoyataka yashughulikiwe ni suala la kukatwa alama tatu kwenye leseni zao za udereva pale wanapobainika kukiuka sheria za usalama barabarani.


Madereva hao wameeleza hayo wakati wakizungumza na One media blog katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Nane Nane jijini Dodoma, ambapo wameiomba serikali kuingilia kati ili kupata suluhisho na kuwawezesha kurejea katika kutoa huduma.


Hatua hiyo imeathiri safari za baadhi ya abiria waliokuwa wakitarajia kusafiri kwenda maeneo mbalimbali, huku baadhi yao wakibaki katika kituo hicho kusubiri hatma ya safari zao.


Abiria hao wameiomba serikali kuingilia kati suala hilo na kuhakikisha suluhisho linapatikana ili huduma ya usafiri iweze kurejea katika hali ya kawaida.







No comments