WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA VIAPO

 


Watendaji wa uchaguzi wamesisitizwa kuheshimu viapo vyao na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Katiba, sheria na kanuni wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao. 

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele, mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi.

Mafunzo hayo ni sehemu ya mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Chamwino Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma na Kata 11 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba, 2026.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata, maafisa uchaguzi, maafisa ununuzi na wahasibu. 

Kata 11 za Tanzania Bara zitakazofanya uchaguzi wa Udiwani ni Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya; Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.  

Nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.









No comments