MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR HEMED SULEIMAN ABDULLA HARIDHISHWI NA HALI YA UCHAFU ULIOKITHIRI KATIKA MITARO

 


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amesema haridhishwi na hali ya uchafu uliokithiri katika Mitaro yakupitishia maji taka iliyopo katika maeneo mengi ya Mkoa wa Mjini Magharibi. 

Ameyasema hayo  leo wakati wa ziara yake ya kukagua Mitaro yakupitishia maji taka iliyopo katika maeneo ya Mfenesi Mazizi, Mayugwani kwa wagonga vyuma hadi TRA , Gulioni mbele ya Ofisi ya zamani ya Mamlqka ya Maji Zanzibar (ZAWA) na Makao Makuu ya Shirika la Umeme zanzibar ( ZECO ).

Amesema hali ya usafi hairidhishi katika maeneo yote aliyotembelea kutokana na kukosekana kwa mipango madhubuti ya kufanyika usafi endelelvu katika mitaro hio ambayo inahatarisha afya za wakaazi wa maeneo hayo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametoa wiki moja kwa Wizara ya ujenzi na uchukuzi kwa kushirikiana na taasisi nyengine kuhakikisha maeneo yote yenye mitaro ambayo maji hayatembei inavyotakiwa inafanyiwa matengenezo ili kuweka mazingira safi na kulinda afya za wananchi katika kipindi hichi cha kuelekea mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha zikiambatana na mvua za ELNINO. 

Amesema katika kupambana na kudhibiti hali ya uchafu katika maeneo mbali mbali ya Mji wa Zanzibar viongozi wanapaswa kushuka kwa wananchi kuwapatia elimu juu ya athari zinazotokana na kuishi katika mazingira machafu yanayoweza kusababisha maradhi ya mripuko ambayo yanaweza kudhibitiwa kwa kujenga tabia ya  kufanya usafi katika maeneo yao wanayoishi. 

Makamu wa pilinwa Rais Zanzibar anaendelea na ziara yake kesho





















No comments