MFANYABIASHARA WICKNELL CHIVAYO AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE ZIMBABWE


Mfanyabiashara maarufu Nchini Zimbabwe, Wicknell Chibayo (SirWicknell), amefariki Dunia leo Septemba 30, 2026 kwa ajali ya ndege binafsi
 iliyotokea katika eneo la vijijini la Marondera,  jiji la Harare nchini Zimbabwe.

Msemaji wa familia ya Chivayo, Herbert Chivayo, pamoja na vyombo vya habari vya kitaifa nchini Zimbabwe kama vile wamethibitisha vifo hivyo. Katika ajali hiyo Chivayo, mke wake, na abiria wengine wote waliokuwemo ndani ya helikopta hiyo wamepoteza maisha.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi na moja jioni (11:00 jioni) kwa saa za Zimbabwe, huku Mamlaka nchini humo bado zinaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo rasmi kilichosababisha helikopta hiyo kuanguka.
Sir Wicknell amefariki akiwa na umri wa Miaka 43. Alikuwa anajulikana barani Afrika kutokana na utajiri wake, biashara zake za nishati kupitia kampuni ya Intratrek Zimbabwe, pamoja na mtindo wake wa maisha ya kifahari na kutoa misaada mikubwa kwa jamii na wasanii.
Siku za hivi karibuni Chivayo na mke wake, walifika Zanzibar Tanzania, kwa ajili ya kumpa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mwenza wake, Mhe. Hafidh Ameir.

No comments