MKURUGENZI MKUU TASAC ATOA SALAMU ZA POLE KWA RAIS SAMIA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Salum, ametoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Hafidh Ameir Hassan.
Bw. Salum akiambatana na Mkurugenzi Huduma za Shirika, Bw. Hamid Mbegu, alitoa salamu hizo za pole, leo tarehe 09 Septemba, 2026, baada ya kuwasili nyumbani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, kwa ajili ya kumfariji na kuungana naye pamoja na familia katika kipindi hiki cha maombolezo.
Aidha Mkurugenzi Mkuu na waombolezaji wengine walitumia fursa hiyo kumuombea dua Mheshimiwa Rais, kwa Mwenyezi Mungu ili ampe subra, imani na nguvu ili aweze kurejea katika majukumu yake ya kuongoza nchi.
Marehemu Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia siku ya Jumatatu, tarehe 07 Septemba, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, na kuzikwa siku hiyo ya Jumatatu, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.

Post a Comment