TANESCO YATANGAZA KUKATIKA KWA UMEME MWANZA, MARA NA SIMIYU
Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO)
limewatangazia wateja wake wa mikoa ya Mwanza,
Mara na Simiyu kuwa kutakuwa na kukatika kwa huduma ya umeme kutokana na
matengenezo katika njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 220
kutoka Shinyanga hadi Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TANESCO leo, Jumamosi,
Septemba 26, 2026, kukatika kwa umeme kutafanyika Jumapili, Septemba 27, 2026, kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa maeneo yote ya mikoa ya Mwanza na Mara, pamoja na baadhi ya
maeneo ya mkoa wa Simiyu, yataathirika
na kukosekana kwa huduma hiyo wakati wa matengenezo hayo.
TANESCO imesema hatua hiyo inalenga kuimarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wateja
katika maeneo hayo.
Aidha, Shirika limewaomba wananchi kutumia tahadhari na
kuendelea kuchukua hatua za usalama wakati wa kukatika kwa umeme.
TANESCO imewataka wananchi ambao watakutana na usumbufu
wowote unaohusiana na huduma ya umeme kuwasiliana na Shirika kupitia namba 180 kwa ajili ya kupata msaada.


Post a Comment