NAIBU WAZIRI CHANDE AKAGUA MAANDALIZI YA SIKU YA UTALII DUNIANI



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amekagua maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani, yanayoadhimishwa kila mwaka Septemba 27.

Mhe. Chande amefanya ukaguzi huo leo, Septemba 26, 2026, katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, ambako maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kesho.

Katika ukaguzi huo, Naibu Waziri amepata fursa ya kuona hatua mbalimbali zilizochukuliwa kuhakikisha eneo hilo linakuwa tayari kwa ajili ya kuwapokea wageni na washiriki watakaohudhuria maadhimisho hayo.

Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa kila mwaka Septemba 27, ikiwa ni siku maalumu ya kuhamasisha umuhimu wa sekta ya utalii katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, pamoja na kuongeza uelewa kuhusu fursa zinazopatikana kupitia utalii.

Maadhimisho hayo pia yanatoa fursa kwa wadau wa sekta ya utalii kujadili namna ya kuendeleza na kutangaza vivutio vya utalii, kuongeza idadi ya watalii na kukuza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa.

Tanzania imeendelea kuweka mkazo katika kutangaza vivutio vyake vya utalii, ikiwemo hifadhi za taifa, maeneo ya kihistoria na kiutamaduni, fukwe pamoja na maeneo mengine

 










No comments