VIONGOZI WAPONGEZA DIRA YA DKT. SAMIA NA MCHANGO WA WANAWAKE.


Wajumbe wa Baraza Kuu, Wenyeviti, pamoja na Makatibu wa UWT kutoka wilaya zote nchini, wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kujionea maendeleo ya utekelezaji wake.


Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary  Chatanda (MCC), ikiwa na lengo la kuwezesha viongozi hao kujionea wenyewe kazi kubwa na maono ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti Chatanda ameeleza kuwa ujenzi wa jengo hilo ni muendelezo wa dira na maono makubwa ya Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuacha alama endelevu ndani ya chama. Alibainisha kuwa wazo hilo lilianzia kwake na kupitishwa na vikao vyote vya maamuzi vya chama kabla ya kuanza kwa ujenzi huo.


Eneo hilo litakuwa na ukumbi wa kisasa wenye uwezo wa kuchukua watu 500. Mradi huo, ambao kwa sasa umefikia takribani asilimia 55, unatarajiwa kukamilika na kuzinduliwa rasmi mwezi Februari, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra na maadhimisho ya miaka 50 ya CCM. 


Mwenyekiti Chatanda amewataka wakandarasi na wasimamizi kuongeza kasi ili kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.


Chatanda amesisitiza kuwa uongozi wa Dkt. Samia tangu aliposhika hatamu za uongozi ni udhihirisho tosha wa uwezo wa wanawake. Alieleza kuwa mafanikio yanayoshuhudiwa yanathibitisha kwamba wanawake wana uwezo mkubwa wa kuongoza na kufanya mambo makubwa bila kutegemea 'kuwezeshwa' tu







No comments