Mama Mariam H. Mwinyi, atoa wito wa kuongeza uwekezaji katika sekta ya mwani
Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam H. Mwinyi, ametoa wito wa kuongeza uwekezaji katika sekta ya mwani kwa kuimarisha uchakataji, kuongeza thamani ya bidhaa na kupanua fursa za kiuchumi kwa wanawake na vijana.
Mama Mariam H.Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 18 Novemba, 2026 wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Uwekezaji wa Mwani Zanzibar (Zanzibar Seaweed Investment Forum), katika Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege , Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema Zanzibar ina zaidi ya wakulima 25,000 wa mwani, ambapo zaidi ya asilimia 80 ni wanawake, hivyo kuna umuhimu wa kuwawezesha kushiriki katika mnyororo mzima wa thamani, ikiwemo uzalishaji, uchakataji, ufungashaji na biashara.
Ameeleza kuwa kupitia ZMBF, taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi, kuongeza upatikanaji wa mitaji na kukuza biashara zinazotokana na sekta ya mwani.


.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment