DKT.MWINYI : SMZ INATAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WA TAASISI ZA KIDINI KATIKA KUDUMISHA AMANI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za kidini katika kudumisha amani nchini.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 06 Januari 2026 alipoizindua Ijitimai ya Kimataifa ya kila mwaka inayoandaliwa na Jumuiya ya Fissabilillah Tabligh Markaz, inayofanyika Fuoni Migombani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amefahamisha kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi pamoja na taasisi za kidini ili kuhakikisha nchi inaendelea kubaki katika hali ya amani na utulivu, huku akiwahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kufahamu kuwa Uislamu unasisitiza elimu, mawaidha na hekima katika maisha ya kila siku.
Aidha, Alhaj Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa jukumu la kuamrisha mema si suala la kuwaachia viongozi wa dini pekee, bali ni jukumu la kila mmoja, na kwamba waumini wana wajibu wa kuhamasishana kutenda mema na kusaidiana.
Post a Comment